Salah aliyekuwa mwiba kwa stars leo alifunga goli la kwana dakika ya 43 kwa mpira wa adhabu nje kidogo ya lango la Stars na kupiga mpira uliomshinda Aishi manula na kuingia mojakwamoja golini.
Muuaji wa Stars Mohamed Salah
Kpindi cha pili kilianza kwa Timu zote kushambuliana kwa zamu na Taifa Stars kufanikiwa kupata penati ambayo ilipaishwa juu na Mbwana Samatta na baadae Salah kuongeza goli la pili baada ya kuwazidi ujanja na nguvu viungo na mabeki wa Stars hadi mwisho wa Mchezo Tanzania 0-2 Misri
Kwa matokeo hayo Misri iliyokamilisha michezo yake kwa kujikusanyia pointi 10 inafuzu kwenye michuano ya AFCON na kuziacha Tanzania na Nigeria zikisuburi kumalizia mchezo wao wa mwisho wa kukamilisha ratiba utakaochezwa Nigeria.

EmoticonEmoticon