MCHEZAJI MAARUFU WA TANZANIA HUKO UK AT CHELSEA AAMURIWA KUKAMATWA NA MAHAKAMA

3:51 AM
MAHAKAMA ya Glasgow’s Justice of the Peace Court ,ya Scotland imetoa hati kwa wanausalama wa nchi hiyo kumkamata na kumfikisha mahakamani hapo kinda wa Chelsea ya England,Islam Feruz,kujibu mashitaka matatu yanayomkabili.

Hati hiyo imetolewa na muendesha mashitaka wa mahakama hiyo Frances McCartney baada ya Ferouz,20, kushindwa kufika mahakamani hapo wakati kesi yake iliipoanza kusikilizwa jana Jumatano Juni 8,2016 kwa kile kinachodaiwa kuwa nyota huyo mwenye asili ya Somalia yuko nchini Tanzania akifanya mazoezi.

Ferouz anakabiliwa na makosa matatu ambayo ni kuendesha gari lake la kifahari aina ya Porsche lenye thamani ya £80,000 wakati akijua fika kuwa amezuiwa.

Kosa la pili aliwadanganya maafisa wa polisi waliomkamata kwa kuwaambia kuwa anaitwa Saeed Cabadalla.Kosa la tatu ni kuendesha gari bila ya kuwa na leseni.

Ferouz alijiunga na Chelsea mwaka 2014 akitokea Celtic ya Scotland.

Share this

SPORT HITS IS A BLOG BASED ON PROVIDING SPORT NEWS FROM ALL AROUND THE WORLD, STAY WITH US ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.. Dont Forget to follow us on Facebook, twitter and Instagram @sporthitstz

Related Posts

Previous
Next Post »