Akizungumza na chanzo kimoja cha habari Jumanne hii, Master J amesema ameamua kusikiliza maombi ya mashabiki wake ambao wamekuwa wakimtaka arudi kwenye game kwa muda mrefu.
“Watu wamenishawishi sana lakini nafikiria, hata Majani tumeongea kwa marefu na naweza sema labda mwaka huu nitarudi, nitakumbushia kumbushia kazi kigogo,” alisema Master J.
Pia mtayarishaji huyo alisema watayarishaji wa muziki wa sasa wananufaika zaidi na kazi zao tofauti na wao ambao walianza kwa kufanya kazi nyingi za bure.

EmoticonEmoticon