JULIO ATENGEWA MILIONI 100 ZA USAJILI

12:58 AM
Kocha wa Mwadui Fc Jamhuri Kihwelu "Julio" ametengewa kitita cha shilingi ,ilioni 100 na uongozi wa Mwadui maalumu kwa ajili ya usajili.
Kiwango hicho ni tofauti na kile cha msimu uliopoita ambapo wadhamini w klabu hiyo walitoa kitita cha shilingi milioni 200 na timu ikamaliza nafasi ya sita katika msimamo wa ligi.
Hii ina maana ya kwamba Julio sasa ashindwe mwenyewe kuitumia vizuri fursa hiyo kusaka nyota watakaopambana na kuibeba Timu hiyo katika msimu ujao.
Timu ya Mwadui imesheheni wachezaji wenye umri mkubwa ambao ni dhahiri inaonekana wapo hatarini kutemwa na kusajiliwa vijana wapya wenye ari zaidi ili kuisadia Timu hiyo iweze kufanya vizuri zaidi msimu ujao.
Source:Mwanaspoti

Share this

SPORT HITS IS A BLOG BASED ON PROVIDING SPORT NEWS FROM ALL AROUND THE WORLD, STAY WITH US ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.. Dont Forget to follow us on Facebook, twitter and Instagram @sporthitstz

Related Posts

Previous
Next Post »