TIMU TATU KUTOKA MKOA MMOJA ZASHUKA DARAJA
kile kitendawili cha nani atashuka daraja hatimae leo kimeteguliwa kwa kushuhudia katika historia ya soka timu tatu kutoka mkoa mmoja kushuka daraja,
Nazizungumzia klabu za Coastal union, Mgambo jkt na African sports zote kutoka katika mkoa wa Tanga zimeshuka daraja kutoka ligi kuu ya Tanzania bara mpaka ligi daraja la kwanza.
COASTAL UNION 0-2 PRISON
hivyo ndivyo walivyomaliza ligi kwa kichapo katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, ingawa tayari Coast walishatoa mkono wa kwaheri mapema na ndio wanaburuza mkia katika msimamo wa ligi hiyo iliyoisha leo
Kikosi cha Coastal union
AZAM FC 1-1 MGAMBO
Haikuwa kazi rahisi uwanja wa chamazi pale Mgambo walipoilazimisha sare Timu ya Azam japo haikuweza kuwasaidia vijana wa Mgambo ambao walihitaji matokeo ya ushindi zaidi, hivyo basi nao kuangukia pua na kuungana na ndugu zao wa Tanga kuiaga ligi kuu
| Kikosi cha Mgambo jkt |
MTIBWA 2-0 AFRICAN SPORTS
Ni kipigo kingine kilichotoa mkono wa kwaheri kwa vigogo wa zamani wa ligi kuu ya Tanzania bara, African sports ambao wangeweza kujikwamua kukutana na kadhia ya kushuka daraja ikitegemeana na matokeo ya mechi nyingine, lakini mpaka refa anapuliza kipenga cha mwisho uwanja wa manungu Mtibwa waliibuka wababe kwa jumla ya magoli 2-0 na kuhalalisha rasmi African Sports kuungana na ndugu zake wawili Coast union na Mgambo jkt zote kutoka Tanga.
kikosi cha African Sports
Jicho lahabari tz inatoa pole kwa wanafamilia wa mpira wa miguu wa mkoa wa Tanga kwa kuondokewa na timu zao zote katika ligi kuu Tanzania bara..

