Wakati Simba ikimaliza msimu huku ikiambulia nafasi ya tatu na kukosa kuukosa ubingwa wa ligi kuu bara pia kutoiwakilisha nchi katika michuano ya kimataifa kwa miaka takribani minne mfululizo, mashabiki wa wekundu hao wa msimbazi wamekuwa na wakati mgumu kuvumilia utani na masimango kutoka kwa wale wenzao wa Yanga.
mmoja wa mashabiki hao na mpenzi mkubwa wa Simba, namzungumzia Bilionea kijana ambaye kwa mara kadhaa amewahi kuifadhili klabu hiyo ya msimbazi Mohamed Dewji maarufu Mo Dewji ameamua kutoa dukuduku lake katika mtandao wa kijamii wa Twitter, jicho la habari tz limenasa comment hiyo ambayo Mo ameeleza hisia zake baada ya simba kumaliza msimu bila ya taji..
Simba imemaliza mchezo wake wa mwisho wa ligi kwa kukubali kichapo cha magoli 2-1 kutoka kwa JKT Ruvu uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

