Mbunge wa Kigoma Mjini na kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe ametumia ukurasa wake wa facebook kuandika mtazamo wake baada ya Rais Magufuli kufanya maamuzi hayo ya kumfuta kazi waziri Kitwanga.
“Uamuzi wa Rais kumfukuza kazi Waziri wa Mambo ya Ndani unatuma ujumbe mmoja – hataki mchezo. Rais amethibitisha kuwa anao uwezo wa kutumbua hata aliowateua. Ni maamuzi muhimu sana kwa Kiongozi wa aina yake. Wale vijana waliokuwa wanatumwa kumtetea wasimame kumtetea. Rais kaonyesha Uongozi ‘ no nonsense “
Ujumbe wa aliyouandika Zitto Kabwe baada ya Rais Magufuli kumfuta kazi aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi Charles Kitwanga
