Mchezaji wa Simba ambaye tayari ameshaonyeshwa mkono wa kwaheri na klabu hiyo Brian Majwega ameamua kumtolea uvivu mganda mwenzake ambae ni kocha wa Simba Jackson Mayanja kwa kumtuhumu kuua kipaji chache.
Akitumia account yake ya kijamii Majwega aliandika,
''Katika maisha tunapitia mengi,Sitaweza kamwe kusahau alichonifanyia mchezaji wa zamani wa kimataifa, kocha Mayanja katika maisha yangu, Namshukuru kwa kuua kipaji changu na kunizungumza vibaya,sijui familia yangu imemkosea nini ila maisha yanaendelea, Namshukuru kwa kunionyesha njia. Mungu mbariki katika kazi yake lakini hatutaweza kamwe kutembea na watu kama hawa katika njia moja'' Aliandika Majwega

