Mchezaji kutoka zesco ya Zambia anaeichezea klabu ya Simba Kwa mkopo alikuwa wa kwanza kuifungia goli Timu ya Simba baada ya kuumalizia krosi ya beki wa Simba Javier Bukungu dakika ya 18.
Dakika ya 28 Ibrahim Ajib aliwainua tena wana msimbazi Kwa kupachika goli la pili akimalizia pasi aliyosetiwa na Laudit Mavugo. . Mpaka timu zinakwenda mapumziko Simba Ilikuwa inaongoza Kwa magoli 2-0.
kipindi cha pili kilianza kwa kasi lakini walikuwa ni Simba waliofanikiwa kupata goli la tatu kupitia kwa Laudit Mavugo katika dakika ya 68.
Kwa matokeo hayo Simba imefikisha alama 51 mbili mble ya Yanga na kurudi katika nafasi ya kwanza waliokuwa wakiishikilia kwa nuda mrefu kabla ya kunyang'anywa na Yanga ambao bado wana mchezo mmoja mkononi.


EmoticonEmoticon