ALIYEKUWA kipa wa Kagera Sugar, Marehemu David Burhan anatarajiwa kuzikwa kesho Jumatano nyumbani kwao Iringa Mjini ambapo leo mwili wake umesafirishwa kutoka Hospitali ya Bungano jijini Mwanza kwenda kwao.
Burhan alipatwa na umauti usiku wa kuamkia jana Jumatano akiwa anapatiwa matibabu kwenye hospitali hiyo ambapo ndugu wa marehemu walidai kuwa ndugu yao aliwataarufu kuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa manjano kabla ya kupatwa na kifo hicho.
Meneja wa Kagera Sugar, Mohamed Hussein ameiambia SPORTHITS kuwa Burhan atakumbukwa kwa mambo mengi aliyoyafanya katika klabu yao pamoja na soka kwa ujumla ingawa kikosi chao kimeshindwa kusafiri kwenda kumsindikiza mwenzao maana hawakujua ratiba sahihi ya mazishi.
"Tulipenda timu nzima ikamzike Burhan ila tulikuwa hatujaambia ni lini familia imeamua kumzika ndugu yetu hivyo wachezaji wawili wameiwakilisha timu ambao ni Babu Ally na Juma Mpola ambao walikuwa rafiki wakubwa wa marehemu na waliishi chumba kimoja.
"Inasikitisha ila hatuna namna nyingine ya kuzuia na tukifika salama basi tumeambiwa kesho tutampumzisha kwenye nyumba yake ya milele Iringa Mjini ambako ndiyo kwao, hapa ndiyo tupo safarini kwenda Iringa," alisema Hussein.
Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahali pema

EmoticonEmoticon