Timu ya Yanga imeanza vyema kampeni zake za kusaka taji la michuano ya mapinduzi baada ya hapo jana kuibamiza bila huruma timu ya Jamuhuri kutoka Pemba kwa magoli 6-0.
Shujaa wa mchezo huo walikuwa ni Simon Msuva na Donald Ngoma ambao wote wawili walifunga magoli mawili kila mmoja huku magoli mengine mawili yakifungwa na Kamusoko na Makapu.
Katika mchezo wa awali Azam waliibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya timu ya Zimamoto.
Ligi hiyo itaendelea leo kwa Simba kukupigia na timu ya kvz usiku ikitanguliwa na mechi baina ya URA dhidi ya Jang'ombe boya utakaochezwa saa kumi jioni.

EmoticonEmoticon