AZAM YAWEKA HISTORIA ZANZIBAR

12:46 AM
Timu ya Azam FC imeweka historia visuwani Zanzibar baada ya timu hiyo kuweka rekodi ya kuwa timu pekee kufika fainali katika Mashindano ya Kombe la Mapinduzi bila ya kuruhusu kufungwa hata bao moja.

Azam wametinga fainali baada ya kuitoa Taifa ya Jang’ombe kwa bao 1-0 katika mchezo wa nusu fainali ambapo katika makundi pia michezo yake yote mitatu hawajaruhusu bao hata moja.

Walianza mchezo wao wa kwanza kwa kuifunga Zimamoto ya Visiwani Zanzibar bao 1-0, wakatoka sare tasa (0-0) na Jamhuri ya Pemba kisha kuifuga Yanga kipigo takatifu cha mabao 4-0, hivyo imecheza michezo yote hiyo bila ya lango lao linaloongozwa na Aishi Manula kuguswa.

Azam FC kesho kutwa Ijumaa January 13, 2017 watacheza Fainali na timu ya Simba mchezo utakaopigwa majira ya Saa 2:15 usiku katika Uwanja wa Amaan.

Hii ni fainali ya tatu kucheza timu ya Azam katika mashindano hayo ambapo aliwahi kucheza mara mbili mfululizo mwaka 2012 na 2013 na zote kufanikiwa kutwaa Ubingwa baada ya kuzifunga timu ya Jamhuri na timu ya Tusker ya Kenya, hivyo ana historia nzuri ya kutopoteza michezo ya fainali katika Kombe hilo.

Share this

SPORT HITS IS A BLOG BASED ON PROVIDING SPORT NEWS FROM ALL AROUND THE WORLD, STAY WITH US ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.. Dont Forget to follow us on Facebook, twitter and Instagram @sporthitstz

Related Posts

Previous
Next Post »