Leo siku ya Jumatano ya Tarehe 28/12/2016 Ligi kuu ya Tanzania Bara inaendelea tena kwa kuzikutanisha Timu za Yanga na Ndanda katika dimba la uwanja wa Uhuru jijini Dar re Salaam.
Yanga wanacheza na Ndanda leo
Bila shaka ni mechi ambayo itakuwa na msisimko wa hapa na pale, wakati Yanga ikitaka kupunguza pengo la pointi na timu inayoongoza katika msimamo wa ligi hiyo Timu ya Simba yenye pointi 41 huku Yanga wakifuatia na poiti zao 37, ni wazi kabisa wanahitaji kushinda mechi hiyo ili kupunguza gepu baina yake na mahasimu wao wakuu Simba.
Ndanda wanacheza na Yanga Yanga leo
Ndanda wenyewe wanaingia katika mchezo huo wakiwa wameshapoteza michezo miwili iliyopita mmoja ni ule waliofungwa na Simba magoli 2-0 na mchezo uliofuatwa wakafungwa na Mtibwa kwa idadi hiyohiyo ya magoli huku wakiwa na kumbukumbu ya kutoka sare na Yanga katika mzunguko wa kwanza katika mchezo uliochezwa Mtwara.
Mojawapo ya mpambano kati ya Yanga na Ndanda
Mchezo wa leo unaelekea kuwa mgumu kwani Ndanda wanapocheza katika uwanja wa Uhuru hubadilika na kucheza kandanda nzuri ya pasi na kushambulia lakini Yanga ambao wametoka kupoteza pointi 2 dhidi ya Afrcan Lyon kwa mchezo ulioisha kwa sare ya 1-1 wataingia wakiwa na hasira huku kocha Lwandamila akitaka kurejesha imani kwa wapenzi wa Yanga.
Pamoja na ugumu wa mcezo wa leo Yanga wana nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi kutokana na ubora wa safu yake ya ushambuliaji na uchu wa kuongeza magoli.
Ndanda wanaonekana kupoteza muelekeo hasa ukichangiwa na ukata ulioikumba klabu hiyo kutoka mtwara.
VIDEO|NDANDA VS SIMBA 0-2



EmoticonEmoticon