JUUKO MURSHID APENYA KIKOSI AFCON CHA UGANDA

3:38 AM
Kocha wa Timu ya Taifa ya Uganda Micho ameteua kikosi cha wachezaji 23 ambao wataiwakilisha Uganda kwenye AFCON ya kwanza baada ya miaka 39 na wanne ni wa akiba iwapo katika orodha ya awali itatokea mmoja ataumia au kupata dharula yoyote kabla ya kuanza mashindano.
Kocha huyo wa zamani wa SC Villa ya Uganda, El Hilal ya Sudan, Orlando Pirates ya Afria Kusini, Yanga ya Tanzania na St George ya Ethiopia, amewataja wachezaji wanne wa akiba ni Watenga Isma, Mukiibi Ronald, Vitalis Tabu na Nsibambi Derrick.
Na kikosi kamili kinachokwenda Tunisia kesho ni; Odongkara Robert, Ochan Benjamin, Jamal Salim Magola, Iguma Denislawyer, Wadada Nicholas, Ochaya Joseph, Batambuze Shafiq, Juuko Murushid, Isinde Isaac na Waswa Hassan. 
Wengine ni Qanyi Timothy, Aucho Khalid, Azira Mike, Mawejje Tony, Kizito Geoffrey, Oloya Moses, Mutyaba Muzamil, Walusimbi Godfrey, Kizito Luwaga Wiliam, Lubega Edrisa, Shaaban Mohammed, Serunkuma Geoffrey, Miya Farouk, Sentamu Yunus, Massa Geoffrey na Onyango Denis.
Uganda, ambayo mara ya mwisho ilishiriki AFCON mwaka 1978 na kuingia Fainali ikafungwa na Ghana 2-0, imepangwa Kundi D pamoja na Ghana, Mali na Misri. 
Kwa ujumla Uganda imecheza fainali tano za AFCON, zikiwemo za mwaka 1962 iliposhika nafasi ya nne, 1968, 1974 na 1976 ilipokomea hatua ya makundi mara zote.

Share this

SPORT HITS IS A BLOG BASED ON PROVIDING SPORT NEWS FROM ALL AROUND THE WORLD, STAY WITH US ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.. Dont Forget to follow us on Facebook, twitter and Instagram @sporthitstz

Related Posts

Previous
Next Post »