Timu ya Azam Fc leo imeendelea kuandamwa na suluhu kwa kulazimishwa suluhu ya goli 1-1 na wenyejiwao timu yaMajimaji ya mjini Songea.
Alikuwa ni Yahya Mohamed aliyeanza kuiandikia timu yake ya Azam goli la kwanza mnamo dakika ya 8 tu ya mchezo huku goli la Majimaji Likipatikana dakika ya 66 ya mcheo huo.
Kwa matokeo hayo Azam imeshushwa mpaka nafasi ya nne katika msimamo wa ligi kuu Bara baada ya kushushwa na Kagera Sugar iliyojikusanyia point 28 na kuiacha Azam na pointi zake 27 huku Simba ikiwa inaongoza ligi hiyo kwa kujikusanyia pointi 41 ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 37.

EmoticonEmoticon