Uongozi wa FC Platinums ya Zimbabwe, umegeuza dili la mshambuliaji Winston Kalengo kutua Yanga baada ya kukataa kulipa mshahara wa Obey Chirwa.
MSHAMBULIAJI WA ZESCO KALENGO
Yanga ilikubaliana na FC Platinums kuwa itampeleka Chirwa kwa mkopo kwa kuwa ilimtoa hapo ili Wazimbabwe wawe wanamlipa mshahara na kama ikitokea dili, wanaweza kumuuza.
“Kweli mwisho ikawa safi na Yanga ikaanza mipango ya kumsajili Kalengo. Kila kitu kimeenda safi na jina limepelekwa lakini inaonekana poa. Lakini mwisho FC Platinums wamekataa kulipa mshahara, sasa inakuwa vigumu kulipa watu wawili.
“Maana Chirwa aende FC Platinums tumlipe, Kalengo naye awe Yanga tumlipe. Imekuwa vigumu na uongozi umetaka kulipa mchezaji mmoja tu, hii imechangia Chirwa kubaki,” kilieleza chanzo.
Yanga ilikuwa imekubaliana kila kitu na Kalengo pamoja na Zesco na lengo lilikuwa ni kuongeza nguvu katika ushambulizi, jambo ambalo linaonekana limekwama.

EmoticonEmoticon