Wanaume waonaofunga uzazi waongezeka nchini

10:26 PM
Siku ya Kimataifa ya Kuhamasisha Wanaume Kufunga Uzazi inadhaamishwa leo duniani kote ambapo hapa nchini idadi ya wanaume wanajiotokeza kupata huduma hiyo imekuwa ikiongezeka
📷Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Marie Stopes Tanzania, Anil Tambay

Siku ya Kimataifa ya Kuhamasisha Wanaume Kufunga Uzazi inadhaamishwa leo duniani kote ambapo hapa nchini idadi ya wanaume wanajiotokeza kupata huduma hiyo imekuwa ikiongezeka ili kuwa na maamuzi sahihi ya kupanga uzazi wa mpango katika familia zao.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirika la Marie Stopes Tanzania kwa vyombo mbalimbali vya habari, takwimu za mfumo wa taarifa za afya za wilaya nchini kwa miaka mitano iliyopita, zinaonyesha kuwepo kwa ongezeko la wanaumewa naofanyiwa njia ya kufunga uzazi, kutoka wanaume wawili mwaka 2011 hadi 905 mwaka 2015, na 1079 kufikia mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu.
Taarifa hiyo ambayo pia imemnukuu Mkurugenzi Mkazi wa shirika hilo TANZANIA, ANIL TAMBAY ambaye amesema njia hiyo ya uzazi wa mpango ni rahisi na haina madhara yoyote kwa mwanaume na kwamba mara nyingi suala la kupanga uzazi limekuwa likionekana kama ni jukumu la wanawake pekee ilhali wanahitaji kushirikiana na wenza wao.

Takwimu hizo pia zinaonyesha kuwa Mkoa wa KIGOMA umekuwa ukifanya vizuri kwa kuwa na mwitikio mkubwa wa wanaume kufunga uzazi, ukifuatiwa na mikoa ya DSM, MWANZA, DODOMA na KAGERA.

Share this

SPORT HITS IS A BLOG BASED ON PROVIDING SPORT NEWS FROM ALL AROUND THE WORLD, STAY WITH US ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.. Dont Forget to follow us on Facebook, twitter and Instagram @sporthitstz

Related Posts

Previous
Next Post »