BLAGNON AANZA MAZOEZI NA WACHEZAJI WENZAKE SIMBA

11:22 PM
Frederic Blagnon akiwa mazoezini
Mshambuliaji Frederic Blagnon amerejea mazoezi katika kikosi cha Simba na kuanza kujifua na wenzake.

Blagnon raia wa Ivory Coast aliikosa Simba katika mechi mbili za mkoani Shinyanga ambako ilikwenda na kuibuka na pointi sita.

Simba ilianza kwa kuitwanga Mwadui FC kabla ya kuimalizia Stand United ambayo haikuwa imewahi kufungwa kwenye uwanja huo, msimu hu.

Blagnon aliungana na wenzake katika maandalizi ya mechi yao ya 14 dhidi ya Africa Lyon kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, leo.

Share this

SPORT HITS IS A BLOG BASED ON PROVIDING SPORT NEWS FROM ALL AROUND THE WORLD, STAY WITH US ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.. Dont Forget to follow us on Facebook, twitter and Instagram @sporthitstz

Related Posts

Previous
Next Post »