BAADA YA KUCHEZEA KICHAPO CHA PILI MFULULIZO, MAYANJA KAYASEMA HAYA

8:23 PM
Baada ya kuchezea kichapo cha bao 2-1 kutoka kwa ‘wajelajela’ wa Mbeya, kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja amesema, walifanya kila wawezalo ili kuondoka na pointi tatu dhidi ya wapinzani wao lakini bahati haikuwa yao.

Kocha huyo mzoefu na soka la Bongo amesema wapinzani wao hawakuwazidi kwa mchezo lakini walikuwa na bahati na walitumia kikamilifu nafasi zao mbili walizozipata.

“Leo hatukuzidiwa sana na Prisons lakini bahati ilikuwa yao kwasababu tumefanya kila kitu lakini wao walikuwa na bahati. Walipata nafasi ya kwanza wakafunga na ya pili pia. Kwahiyo nafasi zao mbili zilimaliza mchezo,” alisema Mayanja baada ya mchezo wa Prisons na Simba kumalizika.

“Hatujamaliza vizuri mzunguko wa kwanza licha ya kuanza vizuri, lakini bado muda upo tunakwenda mapumziko tutafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza ili tukirudi tuendelee kuwa vizuri kama tulivyoanza msimu.”

“Mpira unamambo mengi, kuna wakati unapata matokeo mazuri unayoyahitaji lakini wakati mwingine haiwi hivyo.”
Angalia Goli la Jamali mnyate dhidi ya Prison hapo chini

Share this

SPORT HITS IS A BLOG BASED ON PROVIDING SPORT NEWS FROM ALL AROUND THE WORLD, STAY WITH US ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.. Dont Forget to follow us on Facebook, twitter and Instagram @sporthitstz

Related Posts

Previous
Next Post »