Akihojiwa na Clouds Tv leo asubuhi katika kipindi cha Clouds 360 Zitto Kabwe amesema watanzania wengi wanapenda maendeleo ya vitu kuliko maendeleo ya watu, akihusianisha baadhi ya watu kufurahia kununuliwa kwa ndege za serikali hali ya kuwa wanaanchi wasiokuwa na uwezo wa kupanda hizo ndege wakipata shida za kukosa madawa pindi waendapo hospiali,
Zitto ameshauri Serikali isingetoa kiasi chote cha pesa kununua ndege badala yake ingelipa nusu na pesa nyingine ingeelekezwa kununua madawa na maendeleo mengine ya kijamii.
Pia ameongelea juhudi za Serikali katika kupambana na ufisadi lakini ameishauri kupambana na mafisadi wote wasiwe "selective" katika kupambana na baadhi ya ufisadi na kuacha mwingine akihusianisha kutumbuliwa kwa watu mbalimbali kutokana na kadhia zilizojitokeza huku akikumbushia suala la IPTL na wahusika wake kutokuchukuliwa hatua.

EmoticonEmoticon