TAMBWE HAYUPO KWENYE KIKOSI CHA YANGA DHIDI YA AZAM LEO

5:20 AM
TEGEMEO la mabao la Yanga, Amissi Joselyn Tambwe hayumo kabisa katika mpango wa mchezo wa leo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Azam FC Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Mrundi huyo aliumia katika mchezo uliopita Yanga ikishinda 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro baada ya kugongana na Nahodha wa wapinzani, Shaaban Nditi dakika ya 87 na kushindwa kuendelea na mchezo.

Dawati la tiba la Yanga lilijaribu kupambana kumrejesha uwanjani mapema, lakini imeshindikana na leo kocha Mholanzi amewaanzisha pamoja wachezaji wa zamani wa FC Platinums ya Zimbabwe, Donald Ngoma na Obrey Chirwa mbele ya lango la Azam.

Mzambia Chirwa na Mzimbabwe Ngoma wote walifunga katika ushindi wa 3-1 kwenye mchezo uliopita na leo Pluijm anajaribu tena kushuhudia matunda ya uwili wao.

Kikosi cha Yanga leo ni; Deo Munishi 'Dida', Juma Abdul, Mwinyi Hajji, Vincent Andrew, Kelvin Yondan, Saidi JUma 'Makapu', Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma, Obrey Chirwa na Deus Kaseke.

Katika benchi watakuwapo Beno Kakolanya, Oscar Joshua, Nadir Haroub 'Cannavaro', Matheo Anthony, Mbuyu Twite, Geoffrey Mwashiuya na Juma Mahadhi

Share this

SPORT HITS IS A BLOG BASED ON PROVIDING SPORT NEWS FROM ALL AROUND THE WORLD, STAY WITH US ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.. Dont Forget to follow us on Facebook, twitter and Instagram @sporthitstz

Related Posts

Previous
Next Post »