Timu ya Stand United imeangusha mbuyu mwengine hapo jana baada ya kutoa kicha po cha goli 1-0 dhidi ya Azam fc na kuendelea kuinyemelea Simba kileleni wakijikusanyia pointi 19 moja nyuma ya vinara Simba wene alama 20.
Stand United mpaka sasa wanashika nafasi ya pili na kuonekena kuwa na njaa ya ushindi msimu huu, walifanya hivyo walipoifunga Yanga goli 1-0 na wameendeleza wimbi la ushindi kwa Azam hapo jana.
Kwa jinsi ligi inavyoendelea bila shaka Stand wanastahili pongezi na wanatakiwa kuongeza juhudi ili kuweza kupambana na Top three ambazo kwa miaka mingi zimekuwa ni Yanga,Azam na Simba.
Katika mechi ya jana mashabiki wa Stand walisikika wakishangilia kwamba "Bado simba" hii ni dhahiri vijana wamepania msimu huu..kila la heri stand kwani wadau wa soka wanataka ushindani kama huo katika mpira wa Tanzania.

EmoticonEmoticon