SIRI YA GOLI 5-0 ZA SIMBA DHIDI YA YANGA ZAFICHUKA

11:39 PM
Unakikumbuka kile kipigo cha magoli 5-0 walichokitoa Simba kwa mahasimu wao Yanga, hiyo ilikuwa ni September 11, 2012,ikiwa sasa ni miaka minne tangia kipigo hicho kibaya sana ambacho mpaka leo hakiwezi kusahaulika pale Jangwani kutokea,siri ya kipigo hicho hatimae imefichuka.

Kipigo hicho kilichoongozwa na mshambuliaji wa kutumainiwa wa Simba Emanuel Okwi alitupia magoli mawili na kuchangia kupatikana magoli mengine matatu moja likifungwa na Felix Sunzu kabla ya Juma Kaseja kuifungia Simba goli la nne kwa mkwaju wa Penati na marehemu Patrik Mafisango kuhitimisha karamu ya magoli kwa kufunga goli la tano kwa mkwaju wa penati.

Aliyekuwa kiungo wa Yanga katika mechi hiyo Athumani Iddi Maarufu kama "Chuji" amefichua siri ya kipigo hicho chenye kumbukumbu mbaya kwa Yanga.

Akiongea katika kipindi cha "Morning Trumpet" cha Azm Tv leo asubuhi chuji ametanabaisha kuwa kipigo hicho kilikuwa hakiepukiki na wachezaji walishajua kinachoenda kutokea japo si kwa idadi ile ya magoli.
"Kwa kawaida mechi za Simba na Yanga zinakuwa na maandalizai na motisha mbalimbali kutoka kwa viongozi lakini kuelekea mechi hiyo hakukuwa na motisha yoyote na maandalizi yalikuwa ya kusuasua, viongozi ni kama waliisusa timu" Alisema Chuji.
 Chuji akishuhudia kipa wao akionyeshwa kadi ya nnjano baada ya kumchezea vibaya Emanuel Okwi na kusababisha penati katika mechi hiyo.

Chiji aliendelea kutoboa kuwa wachezaji na benchi la ufundi walikuwa wanadai zaidi ya milioni 30 lakini walilipwa miloni 3 pekee ambazo ziliwashusha morali wachezaji. 

Kama hilo halitoshi Yanga walikwenda Bagamoyo kuweka Kambi ambako napo walijikuta wakikosa mafuta ya kuweka kwenye magari yao kwa ajili ya kurudi Dar es Salaam.

"Gari zilikuwa hazina mafuta na tunatakiwa turudi Dar es Salaam na hakuna dalili za kupata pesa, ilibidi nimpigie mzee wangu mmoja, yeey alinielewa na akanitumia kiasi cha fedha nikamuita kocha na kumueleza na tukaweka mafuta tukarudi Dar es Salaam" Aliongeza Chuji.

Kuelekea mech hiyo Chuji alieleza kuwa wachezaji wa Yanga walikuwa kama Yatima, hawakuwa na mtu wa kuwajali wala kuwasaidia kwa lolote lile, kwa ujumla hakukuwa na maandalizi sahihi kuelekea mchezo huo.

kwa hivyo, sababu kuu ya kipigo kile kilikuwa ni maandalizi duni pamoja na mgogoro uliokuwa unaindama klabu ya Yanga chini ya Nchunga.


Share this

SPORT HITS IS A BLOG BASED ON PROVIDING SPORT NEWS FROM ALL AROUND THE WORLD, STAY WITH US ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.. Dont Forget to follow us on Facebook, twitter and Instagram @sporthitstz

Related Posts

Previous
Next Post »