SIMBA MGUU SAWA, YANGA YALAMBA SUKARI YA MTIBWA

10:20 AM
SIMBA SC imejiweka sawa kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya City jioni ya leo Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Shukrani kwa wafungaji wa mabao hayo Ibrahim Hajib Migomba na Shizza Ramadhan Kichuya, wote kipindi cha kwanza na sasa Wekundu wa Msimbazi wanafikisha pointi 20 baada ya mechi nane
Kwa upande mwingine Timu ya Yanga imezinduka baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ushindi huo wa kwanza ndani ya mechi tatu ikitoka kufungwa 1-0 na Stand United na kulazimishwa sare ya 1-1 na mahasimu SImba SC umerejesha matumaini kwa mabingwa hao watetezi. 
Hadi mapumziko, Yanga walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na winga Mzambia, Obrey Chirwa ambaye leo alichezeshwa kama mshambuliaji pacha wa Amissi Tambwe.

Yanga walifanikiwa kupata bao la pili dakika ya 68 kupitia kwa Msuva kabla ya mshambuliaji aliyetokea benchi Donald Ngoma kufunga la tatu dakika ya 80 akimalizia kazi nzuri ya Mwashiuya. 

Yanga ikalazimika kumalizia pungufu mchezo huo baada ya mshambuliaji Mrundi, Amissi Tambwe kugongana na Shaaban Nditi na kupasuka kwenye dakika ya 87.
Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi 14 baada ya kucheza mechi saba, inazidiwa pointi sita na mahasimu wao wa jadi, Simba SC walio kileleni ingawa wamecheza mechi moja zaidi. 

Share this

SPORT HITS IS A BLOG BASED ON PROVIDING SPORT NEWS FROM ALL AROUND THE WORLD, STAY WITH US ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.. Dont Forget to follow us on Facebook, twitter and Instagram @sporthitstz

Related Posts

Previous
Next Post »