MWANAMUZIKI wa kizazi kipya nchini kutoka kundi la TipTop Connection, Tunda Man amefunga ndoa na mchumba wake wa muda mrefu Bi Sabra, ndoa ya wawili hao imefungwa kwenye Msikiti Mkuu wa barabara ya Boma, mjini Morogoro.
Mkali huyo wa wimbo uitwao ‘Mama Kijacho’ amefunga ndoa hiyo siku ya jana Ijumaa na kuhudhuriwa na baadhi ya marafiki zake wa karibu akiwemo Madee, Dogo Janja na Kassim Mganga. Kabla ya ndoa hiyo kufungwa ilitanguliwa na sherehe ya kuagwa binti ‘Send-off’ iliyofanyika juzi alhamisi.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu aliye mjini Morogoro, sherehe hiyo ya harusi inaendelea kwa siku ya tatu leo nyumbani kwa bibi harusi.






EmoticonEmoticon