Timu ya Yanga inashuka dimbani leo kukipiga na Timu ya JKT Ruvu ikiwa ni siku moja baada ya aliyekuwa Kocha wa Timu hiyo Pluijm kubwaga manyanga kwa sbabu alizodai za kutokuthaminiwa na kushirikishwa katika maamuzi ya kuleta kocha mpya huku yeye akiwa hajapewa taarifa yoyote.
Ni mtihani kwelikweli hasa kwa uongozi wa Yanga ambao unategemea kubebeshwa lawama zote endepo Timu hiyo itafanya vibaya kwani ni majuzi tu Timu ya Yanga iliibuka na ushindi mnono wa magoli 6-2 mjini Bukoba dhidi ya Kagera Sugar chini ya kocha huyo ambae amefanikiwa kuipa Yanga mataji matatu , mawili ya Ligi kuu na Moja la FA, Ngao ya jamii mara moja pamoja na kuifikisha Yanga hatua ya Robo fainali katika michuano ya Klabu bingwa barani Afrika.
Kwa ujumla, Yanga inapindua benchi zima la Ufundi, ikiwaondoa Pluijm na Wasaidizi wake wote, Mwambusi, kocha wa makipa Juma Pondamali na Meneja Hafidh Saleh wote wazalendo na kumpa nafasi Mzambia, George Lwandamina atakayekuwa Kocha Mkuu, akisaidiwa na wazalendo Charles Boniface Mkwasa, Manyika Peter kocha wa makipa na Meneja, Sekilojo Chambua.
Yanga ambao ndiyo mabingwa watetezi, wanashika nafasi ya pili katika Ligi Kuu kwa pointi zao 21 za mechi 10, nyuma ya Simba SC wenye pointi 29 za mechi 11.
GOLI LA TAMBWE DHIDI YA SIMBA YANGA1:1 SIMBA

EmoticonEmoticon