KICHUYA ABADILI UPEPO MSIMBAZI

2:54 AM
Kiungo mshambuliaji wa Simba Shiza Kichuya amebadili upepo wa ufalme Msimbazi,  hapo awali alitazamiwa Mavugo ndio angekuwa mfalme na mrithi sahihi wa Okwi na mtatuzi wa ushambuliaji pale mbele lakini mambo yamekuwa kinyume chake. 

Kichuya ambaye aliaminiwa kuja kuwika Msimbazi lakini si kwa kasi hii ambayo ameibuka nayo na kugeuka kuwa kipenzi namba moja pale Msimbazi. 
Kwa mashabiki wa Simba kwa sasa huwaambii kitu kuhusu kijana huyo aliyetokea Mtibwa Sugar ya Mjini Morogoro. 

Magoli yake mawili aliyofunga moja dhidi ya Azam na lile la kusawazisha dhidi ya mahasimu wa Simba timu ya Yanga,  limefanya watu walisahau jina la Mavugo ambae katika mechi ya watani wa jadi alichemka na kutolewa. 

Mpaka sasa Kichuya ana magoli matano nabkuwa kinara katika msimamo wa ligi na kwa mujibu waaneno yake anataka kufunga zaidi msimu huu ili aibuke mfungaji bora. 

Share this

SPORT HITS IS A BLOG BASED ON PROVIDING SPORT NEWS FROM ALL AROUND THE WORLD, STAY WITH US ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.. Dont Forget to follow us on Facebook, twitter and Instagram @sporthitstz

Related Posts

Previous
Next Post »