Amissi Tambwe awaachia Mashabiki kuhesabu mabao

9:05 PM
MSHAMBULIAJI wa Yanga raia wa Burundi, Amissi Tambwe, amesema hana mpango wa kuhesabu mabao anayofunga Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kwani amewaachia mashabiki kufanya kazi hiyo.

Tambwe ambaye amefikisha mabao 60 katika misimu mitatu ya ligi kuu, amesema hana kawaida ya kuhesabu mabao yake anayofunga kwani amewaachia mashabiki kazi hiyo.

Akizungumza na JICHO LA HABARI jana, Tambwe alisema anayejua zaidi ni Mungu, lakini kwa sasa hawezi kufikiria mwisho wa msimu wa ligi hiyo atafikisha mangapi.

Tambwe alisema hajaweka idadi kuwa atafunga mabao mangapi katika mzunguko wa kwanza au wa pili na ikitokea amefunga anashukuru Mungu lakini hana muda wa kuhesabu hadi atakapomaliza msimu.

Tayari Tambwe amefunga mabao sita katika msimu huu sawa na a Rashid Mandawa wa Mtibwa Sugar huku Shiza Ramadhan ‘Kichuya’ wa Simba akifunga mabao saba.

Share this

SPORT HITS IS A BLOG BASED ON PROVIDING SPORT NEWS FROM ALL AROUND THE WORLD, STAY WITH US ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.. Dont Forget to follow us on Facebook, twitter and Instagram @sporthitstz

Related Posts

Previous
Next Post »