YAMETIMIA| SIMBA YAIKALISHA AZAM KWEUPEEE,KICHUYA AIBUKA SHUJAA

1:08 PM
Shiza Kichuya leo ameibuka shujaa katika mtanange uliokutanisha miamba miwili ya soka nchini Azam na Simba baada ya kufunga goli pekee katika mchezo huo na kuihakikishia Simba kupaa kileleni kwa kujikusanyia pointi 13 ikicheza michezo mitano.
Timu zote zilionekana kucheza kwa ufundi na ushindani mkubwa hususan eneo la kiungo huku Azam wakipata nafasi sawa na zile za Simba lakini umakini ulikosekana katika umaliziaji.
Mpaka timu zinakwenda mapumziko milango ilikuwa migumu.
Azam walianza kipindi cha pili kwa kasi wakilisakama lango la Simba kabla ya kugeuziwa kibao na mambo yakawa ni kupokezana mashambulizi.
Mabadiliko yaliyofanywa na kocha Omong yalionekana kuleta uhai kwa Simba baada ya Ndemla kuingia na kufanikiwa kuongeza nguvu iliyopelekea Simba kupata goli kupitia mshambuliaji wake Shiza Kichuya.

Share this

SPORT HITS IS A BLOG BASED ON PROVIDING SPORT NEWS FROM ALL AROUND THE WORLD, STAY WITH US ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.. Dont Forget to follow us on Facebook, twitter and Instagram @sporthitstz

Related Posts

Previous
Next Post »