Timu za Arsenal, Manchester united,Manchester City, na liverpool za uingereza zimeibuka na ushindi mnono hapo jana dhidi ya wapinzani wao waliocheza nao.
Huko London miamba miwili ya jiji hilo Arsenal na Chelsea walitoana jasho na Arsenal kuibuka na ushindi wa magoli 3-0 magoli yaliyofungwa na Sanchez, Walcot na Ozil
Majogoo wa jiji la Liverpool wameifanyizia Hull city kwa kuitandika magoli 5-1, magoli ya liverpool yalifungwa na James Milner aliyefunga magoli 2 yote kwa mikwaju ya penati, Adam lalana, Sadio Mane, na Cotinho na lile la Hull City lilifungwa na David Meyler.
Baada ya kuandamwa muda mrefu mchezaji ghali Duniani Paul Pogba hatimae ameisaidia timu yake ya Manchester United kuibuka na ushindi dhidi ya mabingwa watetezi leicester City Kw kuifungia goli moja katika ushindi wa magoli 4-1, magoli mengine ya Manchester yamefungwa na Rashford,Mata na Smalling. Na goli pekee la Leicester limefungwa na Demarai Gray.
Manchester City imeendeleza ubabe dhidi ya timu za Uingereza baada ya kuibomoa Swansea magoli 3-1 magoli yaliyofungwa na Aguero aliyefunga magoli mawili na Sterling aliyefunga goli moja na goli la swansea limefungwa na Llorente




EmoticonEmoticon