Dar es Salaam
Rais wa Tanzania John Magufuli jana amefanya ziara Bandarini kukagua utendaji wa kazi na shughuli mbalimbali jinsi zinavyoendelea hapo bandarini.
Rais ameagiza kufanyiwa marekebisho ya mkataba wa kampuni ya Ticts ambayo inajishughulisha kupakia na kuondoa mizigo bandarini, Rais ameagiza kufanyika marekebisho hayo ya mkataba ili uweze kuipa faida Taifa.
Sambamba na hilo Rais ameiagiza mamlaka ya Bandari (TPA) kununua mashine zipatazo ne mahususi kwa ukaguzi wa mizigo inayoingia Bandarini hapo na kumuagiza Waziri husika kushirikiana na TPA kufunga Floor meter ndani ya miezi minne.
Pia ameitaka TPA kujenga Bandari kavu ili kuacha kuzitumia Bandari binafsi ambazo zinatumika kukwepa kodi.
Source:Mwananchi

EmoticonEmoticon