HATARI YA KULA MAYAI YA KUKU WA KISASA

8:02 AM

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema mayai ya kuku wa kisasa yanayotengenezwa nchini yamedaiwa kuwa na mabaki ya dawa ambazo ni hatari kwa afya ya binadamu.

Akizungumza leo wakati alipozindua bodi mpya ya ushauri ya wizara kwa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA), Mwalimu amesema amehakikishiwa na wataalamu hao kuwa dawa zinazotumika kwenye mayai na kuku hao zinabaki ambapo si salama kwa afya ya binadamu.

Mwalimu amesema kutokana na dawa hizo kubaki kwenye mayai na kuku hao ameitaka TFDA kufanya utafiti ili kujua kiwango kipi cha dawa zilizopo ili Serikali iweze kuchukua hatua za haraka.

“Hivyo tuwaachie TFDA waendelee na utafiti wao na wanapobaini ni kiasi gani cha dawa zilizomo kwenye mayai na kuku hao watuambie haraka dawa zipi hazitakiwi na zipi zinatakiwa ili kulinda soko la ndani,”amesema.

Pia amewatahadhalisha wataalamu wa TFDA wasihofie kutoa majibu haraka kwa kufikiri kuwa watakwamisha soko la ndani hivyo wanatakiwa wawe wa kweli ili tatizo lililopo liweze kupunguzwa.

Share this

SPORT HITS IS A BLOG BASED ON PROVIDING SPORT NEWS FROM ALL AROUND THE WORLD, STAY WITH US ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.. Dont Forget to follow us on Facebook, twitter and Instagram @sporthitstz

Related Posts

Previous
Next Post »