STRAIKA WA MEDEAMA KUTUA AZAM FC

7:20 AM
Enock Atta Agyei (kulia) akipambana na Simon Msuva wa Yanga
AZAM FC imefikia makubaliano na klabu ya Medeama FC ya Ghana juu ya kumsajili mshambuliaji, Enoch Atta Agyei.
Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba yupo Ghana kwa ajili ya kukamilisha usajili wa mchezaji huyo na taarifa zinasema ametekeleza jukumu hilo vizuri.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Windy Professionals aliivutia Azam FC akiichezea Medeama wiki tatu zilizopita Dar es Salaam katika mchezo wa Kundi A Kombe la Shirikisho.
Na tangu hapo, Azam FC ikaanza harakati za kuipata saini yake kabla ya jana kukamilisha mpango huo Uwanka wa Essipong Sports mjini Sekondi.

Kinda huyo wa miaka 17, alifunga mabao 17 katika Ligi Daraja la Kwanza ya GN Bank akiwa na Windy Professionals kabla ya kuhamia Medeama SC .
Yanga walishituka kumuona Kawemba katika mazoezi yao Uwanja wa Essipong Sports mjini Sekondi jioni ya jana, wakidhani amekwenda kuwahujumu, kumbe kafuata mchezaji.  

Share this

SPORT HITS IS A BLOG BASED ON PROVIDING SPORT NEWS FROM ALL AROUND THE WORLD, STAY WITH US ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.. Dont Forget to follow us on Facebook, twitter and Instagram @sporthitstz

Related Posts

Previous
Next Post »