Timu ya Chelsea ya uingereza chini ya kocha wake mpya Antonio Conte imekubali kichapo cha magoli 2-0 kutoka kwa wenyeji wao Rapid Vienna katika mechi yao ya kwanza ya kirafiki (Pre-Season) kwa ajili ya maandalizi kuelekea msimu mpya wa Ligi kuu ya Uingereza mwaka 2016/2017.
Angalia picha mbalimbali za matukio katika mtanange huo hapo chini
Antonio conte
Wakati huo huo Timu ya Manchester United chini ya kocha wake mpya mwenye mbwembwe nyingi Jose Morinho imeanza vyema katika mchezo wa kirafiki nyumbani kwa Wigan kwa kuibuka na ushindi wa magoli 2-0.
Morinho katika pozi
Magoli ya Manchester yalifungwa na William Keane dk 49 na Andreas Pereira dk 58.



EmoticonEmoticon