Papa Francis aanguka akiendesha ibada

4:57 AM
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis ameanguka chini wakati akiwa kwenye ibada iliyokuwa ikifanyika katika kanisa la Jasna Gora Monaster kusini mwa Poland.

Akiwa mbele ya madhabahu, kiongozi huyo alishindwa kujizua na kujikuta akiwa chini hali ambayo iliwalazimu wasaidizi wake kumwinua haraka. Tukio hilo

Papa Francis amekuwa akisumbuliwa na tatizo la nyonga ambalo wakati mwingine husababisha maumivu sehemu za mgongo na kushuka hadi miguuni. Hata hivyo, hakupata madhara yoyote na aliendelea na ibada iliyokuwa ikirushwa moja kwa moja na vituo vya televisheni.

Ulinzi umeimarishwa mara dufu nchini Poland kufuatia matukio ya mashambulizi ya mara kwa mara yanayoendelea kushuhudia katika mataifa ya Ulaya. Papa yupo katika ziara maalumu nchini humo na baadaye atasafiri hadi katika mji wa Czestochowa atakokutana na mamia ya mahujaji.

Share this

SPORT HITS IS A BLOG BASED ON PROVIDING SPORT NEWS FROM ALL AROUND THE WORLD, STAY WITH US ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.. Dont Forget to follow us on Facebook, twitter and Instagram @sporthitstz

Related Posts

Previous
Next Post »