Katika mechi hiyo iliyopigwa katika Uwanja wa Chuo cha Biblia cha Highlands cha Morogoro, Simba walionyesha soka safi na la kuvutia.
Raia wa Ivory Coast, Fredric Blagnon ameanza vizuri kwa kupachika mabao mawili sawa na yale ya Ibrahim Ajib.
Wengine waliofunga mabao ni Abdi Banda na Mohammed Mussa Kijiko.
Hiyo ni mechi ya kwanza ya Simba ya kirafiki na ya kwanza kupata ushindi mnono, jambo ambalo litainua morali zaidi ya Msimbazi.
EmoticonEmoticon