Katika kile kinachoonekana ni kutofurahishwa na kitendo cha kunyang'anywa jezi yake namba 9 na kupewa Ibrahimovic, straika wa Manchester United Anthony Martial ameamua ku unfollow account zote za jamii zinazomilikiwa na klabu hiyo zikiwemo Instagram,Facebook na Twitter.
Mabosi wa Manchester United walikubaliana na Ibrahimovic aliyetua Manchester akitokea klabu ya Paris st German ya nchini Ufaransa kuvaa jezi hiyo baada ya yeye mwenyewe kuhitaji namba hiyo ya Martial na kukubaliwa bila kipingamizi.
Kwa mujibu wa habari kutoka RMC Sporsts Manchester United hawakumpa taarifa Martial juu ya jambo hilo bali walifanya maamuzi bila kumshirikisha na kuzua sintofahamu baina ya mchezaji huyo na klabu yake.



EmoticonEmoticon