Katika hali inayoonekana kukamia kunyakua taji la VPL Msimu ujao, Manchester United chini ya Morinho inaonekana kushika kasi katika mbio za usajili kuelekea msimu ujao.
Baada ya kunasa saini ya Ibrahimovic sasa ni zamu ya kiungo mshambuliaji kutoka Borussia Dortmund Henrikh Mkhitaryan pichani juu.
Wakala wa Mkhitaryan, Mino Raiola ameweka bayana kuwa mteja wake atasaini klabu ya Manchester kwa kitita cha Euro M 26 na kuvunja mkataba ambao ulikuwa bado umebaki mwaka mmoja katika klabu yake ya Dortmund.
Mchezaji huyo mzaliwa wa Armeria anaecheza nafasi ya kiungo mshambuliaji alisajiliwa na Dortmund kutoka Shaktar Donesky kwa kitita cha Euro 25 M, mwaka 2013 na amekuwa na mchango mkubwa sana kwenye timu yake.
Swali la msingi ni je? Juan Mata ataendelea kubaki Tranford baada ya ujio wa Mkhitaryan ambae ndio chaguo la Morinho ama la?
Unaweza kuangaliza video za magoli na assist za mchezaji huyo hapo chini


EmoticonEmoticon