Manchester United wapo njiani kutaka kuvunja rekodi ya Dunia kwa kumsajili kiungo wa Juventus Paul Pogba kwa dau la €100m, kwa mujibu wa gazeti la Mail on Sunday Pogba anatarajiwa kulipwa mshahara wa € 250k.
Pogba aliondoka Manchester akiwa na umri wa miaka 19 na kutimkia Juventus mwaka 2012 na kufanikiwa kuitumikia klabu hiyo kwa misimu minne na kupachika magoli 34 katika mechi 178 alizocheza.
Pogba akiwa Manchester United miaka ya 2012 kabla ya kwenda Juventus.


EmoticonEmoticon