Ama kweli Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni..Nadhani mpenzi msomaji utakuwa unahabari juu ya kile kinachoendelea Syria, hata kama si mfuatiliaji wa mambo haya lakini japo juu juu utakuwa umesikia kile kinachoendelea Nchini Syria ambapo kuna vita ya baina ya Serikali na makundi ya waasi kwa zaidi ya miaka 10 sasa. maelfu ya watu wameripotiwa kufa na n alhamisi ya juzi tu watu 15 waliuwawa kutokana na shambulio la serikali dhidi ya waasi.
Katika hali ya kushangaza vijana wa ki sirya wake kwa waume wameonekana katika fukwe za mji wa Latakia, Maili 110 kutoka katika eneo lenye machafuko linaloitwa Aleppo.
Vijana ambao kwa asilimia kubwa walikuwa wamuvua mashati yao na kina dada wakiwa na top zao waliserebuka katika pwani hiyo maarufu kwa jina la Wadi Qandeel beach.
Siku ya pili vijana walionekana wakivuta shisha pamoja na sigara na kuonekana kusahau kile kinachoendelea katika mji wa jirani maili 110 kutoka waliopo.
Haya ndiyo maajabu ya waarabu hawa wa Syria.
Hizi ni picha za juzi tu Alhamisi zikionyesha wahanga wa shambulio la serikali nchini Syria.






EmoticonEmoticon