ZITTO KABWE AITWA POLISI

10:55 PM
Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe jana tarehe 7/6/2016 aliitwa Polisi na Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalumu ya Dar es salaam ACP Camilius Wambura. 

Kwa mujibu wa Katibu Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa chama hicho Ado Shaibu, amesema ACP Wambura amemuita Zitto Kabwe kuhojiwa ikiwa ni siku moja imepita tangu azindue operesheni Linda Demokrasia ambayo inatarajiwa kuzunguka nchi nzima kupinga ukandamizwaji wa Demokrasia nchini 

Amesema licha ya Zitto kuitwa na Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalumu ya Dar es salaam Wambura aliomba Zitto asiende jana kwa kuwa ni karibu na masaa ya kufuturu na kumtaka aende leo saa tatu asubuhi. 

Kwa upande mwingine Shaibu amesema Chama cha ACT-Wazalendo kitawasiliana na wanasheria wao ili kupata tafsiri ya kimahakama ya uhalali wa jeshi la polisi kuzuia mikutano ya vyama vya siasa ambayo inatambuliwa na kulindwa na katiba
source:thechoicetz

Share this

SPORT HITS IS A BLOG BASED ON PROVIDING SPORT NEWS FROM ALL AROUND THE WORLD, STAY WITH US ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.. Dont Forget to follow us on Facebook, twitter and Instagram @sporthitstz

Related Posts

Previous
Next Post »