WAZIRI MKUU WA UINGEREZA DAVID CAMERON AJIUZULU

7:46 AM
Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, ametangaza atajiuzulu, baada ya kushindwa kuwashawishi raia wengi wa Uingereza, kusalia katika Muungano wa Ulaya (EU).

Cameron akiwa amejawa na huzuni amesema kuwa atasalia ofisini kwa siku tisini zijayo ndipo ang’atuke.

Waziri Mkuu huyo aliyeongoza kampeni ya kusalia katika muungano wa EU amesema kauli hiyo imempa mshutuko mkubwa na kwa baadhi ya watu mashuhuri duniani.

Akiongea katika kikao cha waandishi wa habari nje ya afisi yake jijini London, Cameron amesema kuwa hahisi tena kuwa mtu muhimu wa kuliongoza taifa hilo kwa ufanisi chini ya uamuzi kama uliofanywa.

Sauti yake iliibua hisia hasa aliposema "nalipenda sana taifa hili na najihisi vizuri kuliongoza muda huo wote."


Cameron amesema kuwa kauli ya wengi sharti isikizwe japo hafahamu kwanini Waingereza walichukua uamuzi kama huo ilhali taifa hilo lilikuwa linaufanisi mkubwa sana ndani ya EU.


Cameron akiwa ameandamana na mkewe amesema bila shaka sasa utawala mpya unahitajika utakaoweza kutathmini mbinu na mkataba wa kujiondoa kutoka kwa muungano huo wa bara la Ulaya.

Share this

SPORT HITS IS A BLOG BASED ON PROVIDING SPORT NEWS FROM ALL AROUND THE WORLD, STAY WITH US ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.. Dont Forget to follow us on Facebook, twitter and Instagram @sporthitstz

Related Posts

Previous
Next Post »