Timu ya Yanga ya Tanzania imekubali kipigo cha goli 1-0 kutokaa kwa TP Mazembe ya Congo. katika mchezo wa Kundi A, Kombe la Shirikisho Afrika jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Hicho kinakuwa kipigo cha pili mfululizo kwa Yanga, baada ya Juni 19 kufungwa pia 1-0 na wenyeji MO Bejaia 1-0 nchini Algeria.
Shujaa wa Mazembe leo alikuwa ni Mereveille Boppe aliyemalizia mpira wa adhabu uliopigwa na beki Chrtistian Luyindama dakika ya 74.
Katika mchezo huo ambao mashabiki waliingia bure, Mazembe walionyesha kiwango kikubwa zaidi ya Yanga kuashiria kwamba walistahili ushin di huo.



1 comments:
Write commentsNicee
ReplyEmoticonEmoticon