SHILOLE KUTAFUTA MUME KIJIJINI

1:16 AM

Mkali wa Muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amejutia kuwapenda wanaume wa mjini kuwa ni wavivu kila sekta hivyo anajipanga kwenda kijijini kwao Igunga,Tabora kutafuta mume.

Akistorisha na Showbiz Xtra, Shilole alisema kuwa, hataki tena kujichosha akili kwa wanaume wa mjini kwa vile ni wavivu bora aende Igunga kumpata mwanaume atakayeweza kufanya kazi kutokana na vyakula asili anavyokula.

“Wanaume wa mjini wamezoea chipsi mayai, hawawezi chochote bora wa kijijini wanakula dona na wana akili za kufikiria,” alisema Shilole.

Shilole alikuwa akitoka kimapenzi na msanii wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda.
GPL

Share this

SPORT HITS IS A BLOG BASED ON PROVIDING SPORT NEWS FROM ALL AROUND THE WORLD, STAY WITH US ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.. Dont Forget to follow us on Facebook, twitter and Instagram @sporthitstz

Related Posts

Previous
Next Post »