Marekani,
Watu 50 wameuwawa na wengine wengi kujeruhiwa baada ya kijana mmoja Raia wa Marekeni aliyefahamika kwa jina la Omar Mateen (29) kuvamia klabu moja ya mashoga usiku wa kuamkia jumatau.
Omar Mateen
Kijana Omar Mateen aliuwawa na Polisi baada ya mapambano ya Takribani masaa matatu.
Hilo ni tukio baya zaidi la aina hiyo kuwahi kutokea Marekani. Maofisa kwenye hospitali ya Orlando wamedai vifo vinaweza kuongeza. Muda mfupi kabla ya shambulio hilo, Mateen alipiga simu 911 kuelezea utii kwa kundi la ISIS. Baba yake Mateen, Mir Seddique, aliiambia NBC News kuwa mwanae alichukia baada ya kuwaona wanaume wawili wakipigana busu huko Miami miezi kadhaa iliyopita.
Kulikuwa na takriban watu 320 ndani ya klabu hiyo na karibu 100 walishikiliwa mateka.






EmoticonEmoticon