KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Obrey Chirwa amewasili jioni ya leo Dar es Salaam tayari kukamilisha usajili wake kujiunga na Yanga SC.
Chirwa alikuwa mshambuliaji pacha wa Donald Ngoma katika klabu ya FC Platinums ya Zimbabwe.
"Amewasili muda huu, ndiyo nimempokea, tunakwenda kumalizana naye sasa,"amesema Kaimu Katibu wa Yanga, Baraka Deusdedit

Baada ya Ngoma kuhamia Yanga, aliawashauri viongozi wa timu hiyo wamchukue winga huyo wa kulia wa timu ya vijana ya Zambia chini ya umri wa miaka 23.
Na inaaminika Yanga imekubali kutoa zaidi ya dola za Kimarekani 100 000 kuipata saini ya Chirwa ambaye anatokea FC Platinum ya Zimbabwe, klabu waliyotokea wachezaji wake wengine, Wazimbabwe Thabani Kamsuoko na Ngoma.
Mwaka jana, Chirwa alikataa kujiunga na Hobro IK ya Denmark kwa kutoridhishwa na malipo - na maana yake Yanga itakuwa imempa mshahara mzuri.
Yanga inataraka kutuma jina la mchezaji huyo Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ili awahi kucheza mechi za Kundi A Kombe la Shirikisho.
Na mpango huo utafanywa mapema tu atakapokamilisha usajili wake leo akiwasili.

EmoticonEmoticon