Timu ya Taifa ya Italia imeivua rasmi ubingwa Timu ya Taifa ya Hispania kwa kuifunga jumla ya magoli 2-0 katika hatua ya mtoano ya 16 bora.
Giorgio Chiellini akishangilia goli lake
Giorgio Chiellini alianza kuifungia Italia dakika ya 33 ya mchezo.
Wakati mashabiki na pengine hata wachezaji wakiamini huenda mechi itaisha kwa goli hilo moja dakika ya 90 Graziano Pelle aliifungia Italia goli la pili na kuipa mkono wa kwaheri Hispania ambae ndio alikuwa bingwa mtetezi.
Kwa matokeo hayo Italia atakutana na Ujerumani katika hatua ya Robo Fainali.
Baada ya miaka 8 ya utawala wa Ulaya hatimae Hispania imeaga rasmi mashindano ya mwaka huu nhini Ufaransa.
Pelle akifunga goli la pili kwa Italia




EmoticonEmoticon