Klabu soka ya Dortmund ya Nchini Ujerumani imekataa ofa ya Euro 19 M kutoka kwa Manchester United ya Uingereza ofa iliyolenga kumnyakua kiungo wa Brossia Dortmund Henrikh Mkhitaryan.
Wajerumani hao wamesisitiza hawana mpango wa kumuuza kiungo huyo ambae ametoa mchango mkubwa sana kwa Timu hiyo msimu uliyopita kwa kupachika magoli 18 na kutoa pasi za magoli 20 katika jumla ya mashindano yote aliyocheza akiwa na Dortmund.
Kiungo huyo aliyebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake alikuwa anawindwa pia na klabu za Arsenal na Chelsea lakini kwa mujibu wa Agenti wake Mino Raiola amesema mteja wake alipendelea zaidi kutua katika klabu ya Manchester United.
Licha ya Henrikh Mkhitaryan kukataa kuongeza mkataba Dortmund bado wanashikilia msimamo wao wa kutokumuuza kiungo huyo wakiamini ni mtu muhimu kwao na bado wanahitaji huduma yake



EmoticonEmoticon