ABDU KIBA| NIPO TAYARI KUHAMIA WCB

10:13 AM
Abdul Kiba amesema yupo tayari kujiunga na lebo ya WCB inayomilikiwa na Diamond kama hela itawekwa mezani. Bifu la Alikiba na Diamond linaonekana kuathiri mpaka mfumo wa watu wa pembeni wanaowazunguka wasanii hao japo kila mmoja anakubali kuwa hana tatizo na mwenzake huku ukweli wa kila mmoja ukibaki moyoni mwake.

Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo, kinachoruka kupitia EA Radio, Abdu Kiba alisema kuwa kama watakuwa na pesa za kutosha na makubaliano mazuri anaweza kufanya kazi chini la Label hiyo [WCB].

“Nipo tayari naangalia pesa, kama pesa zitakuwepo na wakihitaji kufanya kazi na mimi naweza nikafanya kazi chini ya lebo hiyo,” aliongeza.

Siku chache zilizopita Abdu Kiba ameachia video ya wimbo wake mpya ‘Bayoyo’.

Share this

SPORT HITS IS A BLOG BASED ON PROVIDING SPORT NEWS FROM ALL AROUND THE WORLD, STAY WITH US ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.. Dont Forget to follow us on Facebook, twitter and Instagram @sporthitstz

Related Posts

Previous
Next Post »