WOLPER AWAJIA JUU WADAKU WA PENZI LAKE NA HARMONIZE

5:26 AM

Jacqueline Wolper amewafungukia wanaomsema kuwa haendani na mpenzi wake mpya, Harmonize.

Hivi karibuni familia ya WCB imeonekana kuchafua hali ya hewa mitandaoni baada ya picha zilizokuwa zinasambaa zikionyesha couple hiyo mpya mjini kati ya Jacqueline Wolper na Harmonize huku baadhi ya mashabiki wakisema kuwa ilikuwa ni kiki lakini kwa sasa mambo yanaonekana kubadilika.

Akiongea kwenye kipindi cha Take One, kinachoruka kupitia Clouds TV, Wolper alisema kuwa anaweza akawa na mwanaume anayefanya kazi yeyote sababu haitaji pesa kutoka kwa mwanaume.

“Naweza hata nikawa na mtu anaendesha bodaboda au anaweza sijua akawa mfagia hoteli, sijui anafagia nini lakini mimi kama mimi nikambadilisha na akawa mwanaume wangu. Kwa sababu nachokihitaji mimi sihitaji pesa mimi ni mpiga kazi, mimi nafanya kazi na ndiyo maana mwanzo nimeanza like na fanya promosheni Napata hela yangu, sitaki kutegemea mtu,” aliongeza.

Wolper alianzisha uhusiano na muimbaji huyo wa ‘Bado’ baada ya kuvunja uchumba na mwanaume aliyeahidi kumsomesha nchini Afrika Kusini na ambaye alikuja kugundua kuwa ni mume wa mtu.

Share this

SPORT HITS IS A BLOG BASED ON PROVIDING SPORT NEWS FROM ALL AROUND THE WORLD, STAY WITH US ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.. Dont Forget to follow us on Facebook, twitter and Instagram @sporthitstz

Related Posts

Previous
Next Post »